Mangrove vegetation structure dynamics and regeneration

 

Thesis Philosophiae Doctor Scientiarum

 

Farid Dahdouh-GuebaS


 

Muhtasari

 

Kitabu hiki cha shahada ya juu ya PhD kinajumulisha nakala kumi na nne za taarifa kuhusu mikoko.  Kazi hii ni kilele cha utafiti wangu wa shahada hii iliyo chukua mfululizo wa miaka minne kukamilisha. Kwanza kabisa kuna utangulizi wa utafiti wenyewe.  Utangulizi huu unadokezea madhumini ya utafiti kwa jumla, na umuhimu wake nchini Kenya na ulimwenguni.  Kazi kumbwa ya utafiti huu ilifanyika katika pulu za Mida na Gazi nchini Kenya.  Kazi iliyosalia ilifanyika sehemu za Gale na Pambala nchini Sri Lanka, na pia huko nchini Mauritania katika mbuga ya wanyama iitwayo Aruguini.

 

Utafiti huu umetumia mbinu za kisasa kueleza mambo muhimu katika misitu ya mikoko.  Kwa mfano, jambo la mkusanyiko wa mikoko katika pwani limegusiwa.  Hii ni pamoja na kusahihisha kazi ya hapo awali kuhusu mikoko ya Sri Lanka.  Kwa jumla uharibifu wa misitu uliweza kuoneka katika vituo vya Gazi (Kenya) na Gale (Sri Lanka).  Kituo cha Mida (Kenya) pamoja na kile cha Pambala (Sri Lanka), vilioneka vikiwa katika hali nzuri.

 

Kazi hii inachangia kuonyesha sababu za uharibifu wa mikoko katika nchi hizi, ikiwa pamoja na ukataji mbaya, ukosefu wa mbegu na hali ya kiangazi. Kama mapendekezo wakati wa kupanda mikoko, mwandishi ashauri utafiti kabambe ufanywe kuhuzu upotevu wa mbegu za mikoko kwa njia mbali bali. Pamoja na ukosefu wa mbegu unaotokana na uharibifu wa misitu, kuna uwezekano kwamba mbegu nyini huliwa na wanyama kama vile Kaa pamoja kombe hivyo kuchangia kutonawili kwa mikoko.

 

Katika kituo cha Mauritania, ni kiangazi hasa ambacho kimechangia kudidimia kwa mikoko sehemu ya mbuga ya Aruguini, pwani kaskazini mwa bara la Afrika.  Jambo la wazi ni kwamba eneo hili la Aruguini ndio mpaka wa mikoko kaskazini magharibi mwa Africa. Kunauwezekano kwamba, mabadiliko ya hewa pamoja na ukosefu wa maji baridi yameadhiri sana usitawishaji wa mikoko katika mbuga hii. Anavyo onyesha mwadishi ni kwamba, japo mikoko ina mea kwa shida kule Aruguini, mazao yake hayakuonekana kupunguka.

 

Kwa kumalizia, mwandishi amegusia katika taarifa ya mwisho mojawapo ya taratibu alizo tumia katika utafiti wake. Mwisho kabisa ameunganisha nakala zote kumi na nne akijaribu kujibu swala la jadi kuhusu kusanyiko la mikoko katika pwani.  Je, kwanini Mlilana unaota kado kado ya bahari hali Mchu na Mkandaa inaota katika sehemu karibu na nchi kavu ?

 

Translated by Melckzedeck "Kizzie" Osore, James G. Kairo and Fatuma M. Saidi

 


PhD Table of Contents


Farid Dahdouh-Guebas' Mangrove Biocomplexity Homepage

This page is maintained by Farid Dahdouh-Guebas, fdahdouh@vub.ac.be